Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino kimefanya Mahafali ya kwanza ya Chuo hicho Tawi la Arusha.
Akizungumza Mbele ya zaidi ya wanafunzi 400 wanaohitimu katika mahafali hayo ya kwanza ya chuo hicho Mkurugenzi wa Chuo hicho tawi la Arusha amesema chuo hicho kinafikia Mahafali ya kwanza huku kiwatoa wanafunzi wa Ngazi ya cheti , Stashahada , astashahada, na shah ada ya uzamili.
Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ni Naibu waziri wa Elimu Mh. William Ole Nasha.
Awali uongozi wa Chuo hicho uliipongeza Serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada mbalimbali inazofanya kuboresha sekta ya Elimu.
Aidha wakaiomba serikali kutovitofautisha vyuo binafsi na vyuo vya serikali kwa sababu vyote vinahudumia Jamii ya watanzania.
"Serikali iviangalie vyuo vikuu vyote kwa jicho moja pasipo kutofautisha vyuo vya serikali na vyuo binafsi"
Pamoja na shukrani za chuo hicho kwa Serikali nalo halikusita kuwaasa vijana wanaohitimu kuwa tatizo kubwa la wahitimu ni kushindwa kufanya vitu kwa vitendo badala yake kulalamika ... Wametakiwa kujaribu kufanya Nazi kwa vitendo kuliko kuanza kulalamika.
Suala la Mitandao ya kijamii halikusahaulika ambapo Mkurugenzi wa tawi la chuo hicho akawakumbusha wahitimu kutokuishi maisha ya mitandaoni maisha.
Hata hivyo Mgeni rasmi Naibu waziri wa Elimu William Ole Nasha akawakabidhi vyeti vya pongezi kwa Wanafunzi waliofanya vizuri katika Taaluma
Katika Hotuba yake Naibu Waziri wa Elimu akawataka wanafunzi wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu nchini wawe na maamuzi katika kuchagua vyuo wanavyovitaka kwani imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya wanafunzi wamekwama kuchaguliwa kujiunga chuo kutokana na kuwa wamefanya selection zaidi ya moja.
Nakuweka bayana juu ya iwapo kama serikali imejipangaje kuhusu Sekta ya hiyo nyeti ya Elimu. Mh. Ole Nasha amesema serikali imejipanga kikamilifu kwa kuhakikisha mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu inapatikana kwa wakati huku akiagiza maafisa mikopo kuanza zoezi hilo Mara moja.

Excellent post. I'm facing many of these issues as
ReplyDeletewell..