![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Arusha DC Gabriel Daqarro (Kulia) ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye tukio la Kuadhimisha Siku ya UKIMWI duniani ambapo kwa hapa Arusha imefanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro. |
Maandamano hayo yameanzia Eneo la Halmashauri ya Jiji la Arusha kuelekea viwanja vya Shule Ngarenaro ambako hapo kulifanyika shughuli ya upimaji wa afya kwa wananchi waliofika katika eneo hilo na kupatiwa elimu ya namna ya kuishi na Virusi vya UKIMWI kwa ambao wamepata maambukizi hayo huku jamii ikikumbushwa kutowanyanyapaa wanajamii ambao wamepata maambukizi ya HIV.
![]() |
| Wananchi wakipimwa HIV kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambapo Jiji la Arusha limeadhimisha kwa maandamano hadi viwanja vya Shule ya msingi Ngarenaro. |
Mgeni rasmi katika tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro ambaye katika hotuba yake alisisitiza jamii kuishi na watu kwenye maambukizi ya HIV kwa upendo kwa kutowatenga na unyanyapaa.
Mambo mbalimbali yamefanyika katika Tukio hilo la kihistoria ikiwa ni pamoja na kuhimiza mazoezi kwa jamii na vijana kuachana na maadili yasiyofaa.
![]() |
| Wananchi wakiwa wamejipanga kwenye foleni kwa ajili ya kupima afya. |
Leo dunia inaadhimisha siku ya UKIMWI huku kukiwa na Zaidi ya watu 39,530,090 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na watu zaidi ya 1,540,834 wamefariki kwa Virusi vya UKIMWI. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa tovuti ya takwimu duniani ambayo inaonesha data kamili ambayo ni endelevu.



0 Comments:
Post a Comment