HABARI: Diwani Mchapakazi Melance Kinabo atoa msaada wa Vyoo viwili mahususi kwa Wanafunzi mlemavu

Diwani wa kata ya Themi Melance Kinabo anazidi kujiweka karibu na Wananchi wake jambo ambalo wanasiasa wengi hushindwa kutekeleza pindi wanapopewa majukumu hayo.

Sasa Leo Diwani huyo ametoa msaada wa vyoo viwili vya kisasa ambayo ni Rafiki kwa walemavu.

Mh. Kinabo amemkabidhi Vyoo hivyo Mkuu wa Shule ya Arusha Schools kwa ajili ya kijana ambaye ni mlemavu wa Miguu Ernest Abraham (III) mwenye umri wa miaka 15.

Akizungumza na Habari Tanzania na VOA TV News Bw. Melance Kinabo amesema Mara kwa Mara amekuwa na desturi ya kutembelea Shule za msingi na secondary zilizopo kwenye kata yake hivyo ikawa rahisi kujua uhitaji wa Wanafunzi wake.

Kinabo amesema baada ya kujua tatizo la mtoto huyo ikabidi atafute namna mbadala ya kumsaidia mtoto huyo ambaye hupata shida Saa ya kwenda haja (kujisaidi) hivyo Vyoo hivyo vitamsaidia ambapo choo kimoja kitajengwa sehemu anapolala na kingine Kwenye eneo la darasa anaposoma.

Kijana huyo amekuwa akipata tabu wakati wa haja na amekuwa akitumia Ndoo.

Diwani Kinabo amesema ataendelea  kutoa misaada kama mzazi namba moja wa kata ya Themi ili kuhamasisha jamii na wadau mbalimbali wa masuala ya elimu juu ya Kuona umuhimu wa kuwasaidia walemavu na watu kwenye uhitaji Maalum.
Hivi karibuni Mh. Kinabo alifanya tukio sawa na hilo kwenye Shule ya msingi Themi ambapo kupitia Mdau wa Elimu Mama Isabella Daniel Mmiliki wa Shule ya Upendo Friends alijenga vitundu sita vya choo vya wanafunzi walemavu wa macho.

0 Comments:

Post a Comment