KINABO Kawahimiza Wananchi Kushiriki katika Shughuli za Maendeleo

Diwani wa Kata ya Themi Mh. Melance Kinabo

Wananchi waliohudhuria mkutano wa kikao cha wazazi shule msingi Themi

Hivi karibuni kumefanyika kikao cha Wazazi na Kamati  ya shule ya Msingi Engira iliyopo kwenye Halmashauri ya Jiji la Arusha kikao alichoshiriki pia Diwani wa kata hiyo Melance Kinabo ambaye pia ni mwanakamati.

Kwenye kikao hicho yamezungumzwa masuala mengi ikiwemo changamoti ya Baadhi ya wazazi kugomea kulipa fedha za mchango kwa ajili ya mlinzi wa shule na Pesa kwa ajili ya Mpishi na kuni licha ya Diwani kuwapatia mfadhili ambaye anawapatia chakula na maji ya kunywa wanafunzi zaidi ya 700 kwa siku mwaka mzima.

Kamati ya shule hiyo pamoja na wazazi kikaamua kuwa wazazi ambao wataendelea kugomea maazimio hayo ambayo ni kiwango cha Shilingi 2000 kwa mwezi (Tsh.100 kwa siku) wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu  pamoja na kuhojiwa kwenye Kamati ya shule ili kufahamika kama hawana uwezo au ni kiburi.

Kwa upande wake Diwani Kinabo akasema endapo itabainika kuwa wazazi hao hawana uwezo Kamati itachukua jukumu la kuwasaidia wazazi hao hivyo itakuwa ni njia rahisi kubaini hali ya maisha yao.

Katika hatua nyingine Kinabo aliwataka   Wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ya Shule hiyo kwa manufaa ya watoto wao na kizazi kijacho.

Mh. Kinabo amesema kamati ya shule hiyo inatarajia kukarabati choo bora katika shule hiyo Ukarabati ambao unategemewa kugharimu Fedha zaidi ya Tsh. Million mbili (2.4 Million) ambazo ni jitahada za Diwani wa kata hiyo , michango ya wananchi , na kamati ya shule.

Hata hivyo Mh. Kinabo aliwahimiza wazazi katika kikao hicho kuchangia fedha kiasi Taslim Tsh. 2000 kwa kila mzazi ili kupata Shilingi laki saba (700,000) kufikia lengo la Tsh. Million 2.4 baada ya Diwani kukabidhi baadhi ya fifaa kwenye shule hiyo ikiwa ni pamoja na Milango, Tolilet Sink , Tapes na Mfumo  wa mipira ya kusambazia maji.

Hadi kikao hicho kinaisha maazimio kadhaa Yote yamefikiwa na wazazi kuafiki kulipa Fedha kwa ajili ya mlinzi , Mpishi wa shule na Mchango kwa ajili ya ukarabati wa Choo.

0 Comments:

Post a Comment