BAVICHA NA UV CCM WAZIDI KUTUNISHIANA MSULI,WANATAKA SHAKA AACHE KIJIKOMBA




Baraza la vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Manyara
 tumeshtushwa na kusikitishwa na kauli zilitolewa na kiongozi mmoja wa UVCCM Ndugu Hamidu Shaka, ambaye hivi karibuni amenukuliwa na vyombo vya habari akitoa matamshi yanayoashiria chuki na nia mbaya kwa Raisi wa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) ambaye pia ni Mh Mbunge wa Singida Mashariki, mwanasheria Mkuu wa Chadema mh Tundu Lissu. 

Wakati Mwingine amenukuliwa akiwa Singida akitutishia sisi vijana wa Baraza la Vijana wa Chadema(BAVICHA). Haijulikai Shaka katumwa na nani au anafanya yote haya ili kujikomba kwa Nani. Tabia hii ya kijana Shaka inadhihirisha Aina ya siasa za kujikomba Kama siyo kujipendekeza ambazo zimekuwa zikifanywa na vijana wa UVCCM ili kuokoteza umaarufu wa kisiasa kupitia majina ya watu!


Kwa nia njema kabisa tunamwonya kuacha tabia hiyo na tunamshauri Ndugu Shaka mambo yafutayo:

1. Ndugu Shaka Hana hadhi ya kubishana na Lissu, na ushahidi wa hilo, hadi sasa chama chake chenyewe kimeshindwa kumwamini ndo Maana ameishia tu kukaimu nafasi ya Katibu mkuu hadi leo.

2.  Bavicha tulitegemea Shaka aungane na akina MacDonald wa Jimbo la Kinondoni kudai na kupinga Uvunjwaji Katiba unaofanywa na Mwenyekiti wao wa CCM kwa kuwanyima wanachama wa CCM haki za kikatiba za kushirikishwa,  kuchagua na kuchaguliwa ndani ya Chama Chao!

3. Awaongoze Uvccm kudai haki ndani ya Chama Cha CCM haki ya wagombea uenyekiti na Makam kushundanishwa badala ya kupitishwa bila kupingwa na bila kujaza fomu ya kuomba kugombea.

 4 . Aiombe  Serikali yake  kuamka na kuchukua hatua stahili kuzuia vitendo vya utekaji kwa wanahabari na wanasiasa wa Upinzani Pamoja na kuimarisha usalama wa raia na mali zao,

5.Shaka angetumia huo muda wake kuishauri serikali ya chama  Chake  kuwajengea vijana uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi, kuwapa fursa ya Elimu bora, mazingira bora ya Upatikanaji wa Ajira,

Ndugu Shaka akizingatia Ushauri huu unaweza ukafanya angalau kuaminiwa na Mwenyekiti wake wa chama na si kwa ngonjera anazofanya sasa.

Tunamwonya Shaka na vijana wengine wa aina yake kuwa wasithubutu kututisha Bavicha! Bavicha ni sauti ya vijana nchi nzima.

Kama anataka kupambana na Bavicha amshauri Mwenyekiti wake wa CCM aruhusu mikutano ya hadhara tukapambame jukwani! Kinyume na hapo Bavicha tunamwona Shaka Kama mtu asiyejitambua, amepoteza mwelekeo na anayeiabisha Uvccm kwa malumbano yasiyo na tija!

Bavicha mkoa wa Manyara tunapenda kuwasisitiza vijana wote tuendelee kuunganisha nguvu zetu kudai utawala wa sheria, unaozingatia Haki za binaadamu katika taifa letu, sisi vijana tuna kesho nyingi kuliko jana hivyo amani katika taifa hili ni muhimu Sana kwetu, ukizingatia kuwa Haki ndo tunda la Amani, hivyo tuna kila sababu ya kuhimiza kutendeka kwa Haki katika taifa letu.

Frank Oleleshwa
Mwenyekiti wa Bavicha
Mkoa Manyara
12/01/2018.
Babati.

0 Comments:

Post a Comment