Huu utakuwa mradi kwanza kwa mwaka 2018 toka mwaka huu uanze.





Diwani wa Kata ya Themi Mh. Melance Kinabo kwa kushirikiana na Diwani mwenzake wa kata ya Lemara Profesa Sambuli Mosha na Halmashauri ya Jiji la Arusha mgeni rasmi akiwa Mkurugenzi Athumani Kihamia wamezindua mradi wa kivuko cha watembea kwa miguu na magari hadi tani 7.
Mradi huo umegharimu zaidi ya Millioni 7.
Kivuko hicho kinawasaidia wakazi wa mtaa wa Themi mashariki kwenye Kata ya Themi na Mtaa wa Lemara kati kwenye Kata ya Lemara.
Kinabo Anasema huu ni mradi wa kwanza kwa Wananchi wake wa Themi kwa mwaka huu mpya 2018 huku akibainisha changamoto zilizokuwepo wakati mradi huo ulikuwa bado kukamilika. Na kwamba sasa hii imekuwa mwarobaini wa Tatizo hilo.
Kwa kipindi kirefu wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata shida kufikia huduma ya Afya , ibada na masuala mengine yahusuyo jamii. Zaidi play hii video hapa chini
MIKUSANYIKO YA PICHA ZOTE







0 Comments:
Post a Comment