KINGUNGE ANENA MAZITO, AMUONEA HURUMA LISSU


MWANASIASA mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ameonyesha hisia zake juu ya maumivu makali ya majeraha ya risasi anayoyapitia mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.


"Wakati madaktari wananisafisha haya majeraha nikawauliza, kama mimi nasikia maumivu hivi Lissu je ana maumivu kiasi gani?" amehoji Kingunge.

Ameyasema hayo leo wakati mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe na waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa walipombelea kwenye ya hospitali ya taifa Muhimbili anakopatiwa  matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na mbwa wake.

Hali ya mwanasiasa huyo mkongwe inazidi kuimarika na anatarajia kutoka hospitalini hapo hivi karibuni ili kushiriki mazishi ya mkewe yanayotarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es salaam.

0 Comments:

Post a Comment