MBOWE, LOWASSA WAMJULIA HALI KINGUNGE LEO



 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe na waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa wamemtembelea hospitali mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Viongozi hao kutoka chama kikuu cha upinzani nchini wamemtembelea Kingunge  leo kwenye ya hospitali ya taifa Muhimbili anakopatiwa  matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na mbwa wake.

Hali ya mwanasiasa huyo mkongwe inazidi kuimarika na anatarajia kutoka hospitalini hapo hivi karibuni ili kushiriki mazishi ya mkewe yanayotarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es salaam.




0 Comments:

Post a Comment