Katibu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Tarime, Tobias Ghati, amejivuwa uwanachama wa chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi, (CCM).
Tukio hilo llililopokewa kwa hisia tofauti na wananchi hasa wafuasi wa Chadema limetokea leo mchana mjini Tarime mkoani Mara.
Katibu wa Chadema mkoani, Mara, Chacha Heche alilishutumu jeshi la polisi Kwa madai kuwa limehusika kumtisha kiongozi huyo ili ajiuzilu.
"Kitendo cha jeshi la polisi Tarime Rorya, kumkamata Thoius Ghati ( Katibu wa Chadema wilaya ya Tarime na kushinikiza na viongozi wa CCM kumshawishi kukiri makosa ya matumizi mabaya ya mtandao ama kujiunga na CCM kwa kushirikiana na familia yake sio kuidhofisha CHADEMA ni kuonesha uwezo mdogo wa kushawishi watu
Badala yake sasa mnatumia dola kulazimisha watu waone kuwa ccm inakubalika," ameandika Heche kwenye ukurasa wake wa face book
Aidha alidai kuwa kitendo hicho ni udhaifu mkubwa na hautawajenga CCM bali utawabomoa.
Huyu no kiongozi wa pili wa CHADEMA kujiuzulu wilayani humo baada ya aliyekuwa diwani wa kata ya Ture, Zakayo Chacha Wangwe kujiuzulu.

0 Comments:
Post a Comment