SERIKALI KUNUNUA VICHWA 25 VYA TRENI, TANZANIA MIONGONI MWA NCHI TANO BORA KIUCHUMIA AFRIKA, VIWANDA ZAIDI YA 3,000 VIMESAJILIWA

MKURUGENZI MKUU, IDARA YA HABARI - MAELEZO NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, DKT. HASSAN ABBASI ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO AMEFANYA KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI NA KUELEZA


#Natoa rai kwa waandishi kuanza kuleta maombi kwa ajili ya vitambulisho vya wanahabari vya mwaka 2018 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Pia natoa rai kwa Waandishi wa Habari kushiriki katika tuzo za wanahabari za SADC na UNESCO ambazo zitapatikana kwenye tovuti ya Idara ya Habari - MAELEZO- Dkt. Hassan Abbasi.

#Nidhamu mpya katika ukusanyaji na matumizi ya fedha za umma pamoja na dhamira ya dhati ya kutekeleza ahadi vimeisaidia kuongeza kasi ya utekelezaji miradi - Dkt. Hassan Abbasi.

#Tunaendelea kuwahakikishia wananchi kuwa hali ya uchumi wa nchi yetu inaendelea kuwa imara - Dkt. Hassan Abbasi.

#Ripoti ya Shirika la Fedha Duniani, Benki ya Dunia na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani zimetabiri kuwa wakati uchumi wa Dunia utakuwa kwa wastani wa asilimia 4 kutokana asilimia 3.7 means Jana ukuaji wa uchumi kwa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 kwa mwaka 2018 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Ukuaji huo wa uchumi unatajwa unaiorodhesha Tanzania kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika - Dkt. Hassan Abbasi.

#Ahadi ya kuhamia Dodoma, jumla ya wafanyakazi 3,671 kutoka wizara na taasisi mbalimbali za umma wameshahamia Makao Makuu Dodoma - Dkt. Hassan Abbasi.

#Awamu itakayofuata baadaye mwaka huu  itahusisha wafanyakazi wengine 2, 460 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Natoa rai kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa zitokanazo na uhamiaji wa wafanyakazi wa umma katika Makao Makuu Dodoma - Dkt. Hassan Abbasi.

#Kuhusu viwanda, kufikia mwaka jana viwanda zaidi ya 3,300 vilisajiliwa - Dkt. Hassan Abbasi.

#Ujenzi na uzalishaji katika viwanda hivyo uko katika hatua mbalimbali - Dkt. Hassan Abbasi.

#Kati ya miradi iliyosajiliwa, viwanda vikubwa ni 652 vyenye jumla ya mtaji wa shilingi trilioni 5 utakaowekezwa nchini na vitaajiri wafanyakazi 50, 625 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Katika miradi ya umeme Serikali inaendelea kutekeleza miradi zaidi ya 20 ya kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika - Dkt. Hassan Abbasi.

#Miongoni mwa miradi hiyo ni usimikaji wa mitambo ya umeme wa gesi Kinyerezi I na II ambapo mitambo hiyo itaongeza Megawati 425 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Wakati mtambo wa Kinyerezi I wa nyongeza umefikia asilimia 50, mtambo wa Kinyerezi II umekamilika kwa asilimia 87 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Mnamo Desemba, 2017, mtambo wa Kinyerezi II umeingiza Megawati 55.94 katika Gridi ya Taifa na kiasi kingine cha Megawati 27.94 kinatarajiwa kuingia kwenye gridi mwezi huu- Dkt. Hassan Abbasi.

#Mitambo yote miwili inatarajiwa kukamilika mwaka huu - Dkt. Hassan Abbasi.

#Serikali imeendelea kutekeleza ujenzi wa reli ya kisasa kwa kuanzia kipande cha Kilometa 300 Dar es Salaam - Morogoro kitakacho gharimu trilioni 2.7 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Usanifu wa njia itakayopita reli umeshakamilika, kwa sasa uandaaji wa tuta na ujenzi wa madaraja umeanza kwa kasi - Dkt. Hassan Abbasi.

#Pia mkandarasi ameshaanza maandalizi ya ujenzi wa kipande cha pili cha kilomita 442 Morogoro - Dodoma kitakachogharimu trilioni 4.3 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Serikali kupitia Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli imeshatangaza zabuni zitakazofunguliwa mwezi huu kwa ajili ya kupata makampuni yatakayotengeneza vichwa vya mabehewa ya kisasa ya treni ya umeme na mafuta - Dkt. Hassan Abbasi.

#Katika zabuni hiyo Serikali inatarajia kununua vichwa 25, mitambo 25 ya ukarabati wa reli na mabehewa 1, 590 - Dkt. Hassan Abbasi.

#Kati ya mabehewa hayo, 1,530 ni ya mizigo na mabehewa 60 ni ya abiria ambapo 15 ni daraja la kwanza na 45 ni daraja la kawaida - Dkt. Hassan Abbasi.

#Katika Ziwa Nyasa meli mbili mpya za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma zinazobeba mizigo tani 1,000 zimeanza safari kwenda bandari mbalimbali - Dkt. Hassan Abbasi.

#Meli nyingine mpya ya abiria inategemea kukamilika mwezi Juni mwaka huu - Dkt. Hassan Abbasi.

#Katika ziwa Victoria, Mkandarasi wa kutengeneza meli mbili kubwa, mpya na za kisasa ameshapatikana - Dkt. Hassan Abbasi.

*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO.*

0 Comments:

Post a Comment