![]() |
| Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha (katikati) Elias Mungure. Picha VOA TV News |
1. Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure amekemea vikali utaratibu wa ukiukwaji wa Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika baadhi ya vipengele hasa vipengele vinavyohusu Vyama vya siasa kwa haki ya Mikutano ya siasa , maandamano na Uhuru wa mawazo.
Mungure ameyasema hayo mapema hii Leo wakati akizungumza na vyombo vya Habari ambapo amesema katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikivunjwa na viongozi wa serikali. tazama video hii hapa chini.
2. Katika hatua nyingine Mungure ameitaka Serikali ya Tanzania kuiga mfano wa Nchi nyinginezo za mfumo wa vyama vingi kwakuwa zimekuwa zikiheshimu vyama vya siasa na kumtaka Rais Magufuli kuwaacha Wafanye mikutano ya Siasa. Tazama clip hii fupi ya video.
3. Vilevile Mungure akadai Katiba mpya kwa kueleza umuhimu wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi huku akimshtumu vikali Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Mh. Humfrey Polepole kwa madai kuwa amewasaliti wadai wa katiba mpya kwani alikuwa miongoni mwa watu waliodai katiba mpya.. Tazama hii video fupi..

0 Comments:
Post a Comment