Mwenyekiti wa Husea, Renny Chiwa,akiwasilisha mada juu ya makazi
holelaTanzania,katika semina ya mafunzo ya siku moja kwa wataalamu wa mipango miji wa halmashauri ya Jiji la Arusha na madiwani wa halmashauri hiyo
WATAALAMU wa mipango miji katika Halmashauri ya Jiji la Arusha,wametakiwa kupima maeneo ambayo hayajavamiwa na wananchi ili kutekeleza mpango wa kupunguza makazi holela nchini.
Ushauri huo ulitolewa januari 29, mwaka huu na Mratibu Mkuu wa miradi ya Kamouni ya Upimaji na Upangaji wa Makazi(Husea),Edward Kinabo,akipokuwa akitoa mafunzo ya siku moja kwa wataalamu aa mipango miji na madiwani wa halmashauri hiyo.
Alisema ili kupunguza ujenzi holela wataalamu hao kwa kushirikiana na madiwani hao wanapaswa kuelimisha wananchi juu ya urasimishaji ili watambue fursa mbalimbali za kimaendeleo zilizopo kupitia mpango huo.
Alisema katika mkoa wa Arusha kuna tatizo kubwa la wananchi wengi kuishi katika makazi holela ikiwa ni pamoja na kata za Sombetini,Themi,Elerai,Olasiti na Daraja Mbili,hali inayochangia msongamano mkubwa na kukosekana kwa huduma za kijamii.
"Wataalamu kwa kushirikiana na madiwani mnapaswa kuhakikisha maeneo ambayo bado watu hawajaanza kuishi mnayapayima,yajulikane ni kwa ajili ya matumizi gani ili yasiharibike na kupunguza makazi holela,na kuwapatia hati miliki ili waweze kuzitumia kupata mikopo na kuanzisha miradi ya maendeleo,"alisema na kuongeza
"Lengo la semina hii ni kuwapa elimu kuhusu miradi ya kupanga miji, kupima na kumilikisha ardhi,ili kubadili jiji la Arusha kwani mtu akikosa hati miliki anakuwa na mtaji mfu,wengine wanadhulimiwa ila mkipanga na kutoa hati mtaweza kupunguza migogoro ya ardhi,"
Awali Mwenyekiti wa kampunk hiyo, Renny Chiwa,alisema katika zoezi hilo la upimaji unafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya ndege(drones) zinazotumika kupiga picha na kuainisha maeneo.
Alisema wataalamu wana wajibu wa kutoa elimu,kuzuia ujenzi holela ambao una athari nyingi ikiwemo kuchangia magonjwa ya milipuko,kukosekana kwa huduma za jamii,migogoro ya ardhi,kukosekana kwa mapato,hali mbaya ya maji taka na migogoro ya ardhi.
"Lengo la mradi wetu ni kupunguza makazi holela na kurasimisha makazi,kuokoa maeneo muhimu kwa ajili ya huduma za kijamii,kusaidia ongezeko na ukuaji wa miji na kuwawezesha wananchi wa hali ya chini,kati na juu kuwa na maeneo salama"alisema
Kwa upande wao baadhi ya madiwani hao walisema ni muhimu wataalamu wa upangaji miji kutoa elimu zaidi kwa wananchi juu ya miradi ya upimaji,upangaji na urasimishaji wa maeneo ya makazi.
Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(Chadema),alisema sekta binafsi katika swkta ya ardhi na mipango miji itasaidia kupunguza makazi holela katika maeneo mengi hapa nchini.
"Elimu hii ni nzuri hivyo na sisi kama madiwani tuko tayari kazi ni kwa ofisi ya Mkurugenzi ione nini tunaweza kufanya tupeleke sehemu sahihi ya kutolea maamuzi ili tuangalie uwezekano wa kutumia elimu tuliyopata kupunguza makazi holela,"aliongeza

0 Comments:
Post a Comment