ASKOFU KKKT AOMBA RADHI AWAANGUKIA WAUMINI WAKE A



Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki, Dk Lucas Mbedule amewaomba radhi waumini wa dayosisi hiyo na Baraza la Maaskofu kwa kutokusoma waraka uliotolewa wa sikukuu ya Pasaka.
Askofu Mbedule ameomba radhi leo Aprili 29, 2018 wakati wa Ibada ya iliyofanyika kanisa la Mtwara Mjini, amesema licha ya salamu hizo kutokusomwa, anaunga nazo na yupo pamoja na maaskofu wenzake.
Akisoma barua ambayo ameituma kwa Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo na maaskofu wote wa kanisa hilo, Askofu Mbedule amesema baraka za ma-baba maaskofu zilishindwa kusomwa kwa sababu zilizojitokeza wakati huo.
“Kwa njia ya barua hii, kwanza napenda kuwaombeni radhi kwa kuwakosesha baraka za baba maaskofu,” amesema Askofu Mbedule.
Amesema yeye alishiriki kuuandaa na kutia saini na yupo pamoja na maaskofu wenzake.

Hatua hiyo imekuja baada ya baraza hilo kuwaweka kando maaskofu wake watatu wa kanisa hilo Kwa madai ya kujitenga na waraka huo.

0 Comments:

Post a Comment