HIDAYA WA PEPE KALLE ANENA MAZITO BAADA YA MWANAWE KUZIKWA

Hidaya Mtumwa akiwa na mwanawe,  Marehemu Leyla  enzi za uhai wake 

Mama yake marehemu Leyla, Hidaya ameiomba serikali isaidie kuhakikisha aliyehusika na mauaji ya binti yao analetwa nchini ili waweze kuifuatilia kesi inayomkabili kwa ukaribu na kujua hatma kwani kwa sasa itawawia vigumu kufuatilia nchini Uingereza inapoendelea kutokana na umbali.

Hidaya aliyasema hayo akiongea na waandishi wa habari Nyumbani kwake Kaloleni baada ya mwili wa marehemu Leyla kuondolewa nyumbani hapo kwa ajili ya kwenda kufanyiwa dua Msikiti wa Nuur kisha kwenda kuzikwa Sinon kwenye makaburi ya familia hiyo.

Hidaya ambayo ni mfanyabiashara  aliyekuwa maarufu miaka ya nyuma  baada ya kuimbwa na mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kabasele Yampanya maarufu Pepe Kalle katika wimbo wake wa mwaka 1991, 'Hidaya!'.
Kwa upande wa familia ya mume wa marehemu Leyla, Lema maarufu Belly, Kasambula Kema maarufu 'Skassy Kasambula,' alikuwa mwanamuziki nyota nchini Tanzania  kabla ya kuhamia Nairobi.
Mama yake Belly, Bishada aliwahi kuimbwa mwaka 1981 katika wimbo 'Bishada' uliorekodiwa na Bendi ya Super Matimila na baadaye katika wimbo 'Mama Belly,' wa Bendi ya Sambulumaa mwaka 1989.

0 Comments:

Post a Comment