MAZIKO YA MTOTO WA HIDAYA WA PEPE KALEE

MKUU wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameongoza waombolezaji kwenye dua na  maziko ya Leyla Mtumwa aliyefariki nchini Uingereza kwa kushambuliwa na kitu chenye ncha kali na mume wake, Kema Kasambula Machi 30, mwaka huu.




Leyla aliswaliwa kwenye msikiti wa  Nuur wa Kaloleni kabla ya kwenda kuzikwa kwenye makaburi ya familia yaliyopita Sinoni.



Dua na mawaidha ulifanyika nyumbani kwa mama wa marehemu Leyla, Hidaya Mtumwa mtaa wa Kaloleni na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

Mama wa marehemu Leyla, alipata umaarufu alipotungiwa wimbo na mwanamuziki wa Zaire, sasa Demokrasia ya Congo, Pepe Kalle.



Awali sheik Rajab Kiungiza akitoa mawaidha akiwahimiza waombolezaji kufanya toba wakiwa hai kwani  nafasi hiyo hawataipata wakiwa wamekufa.

Leyla Mtumwa enzi ya uhai wake


Aidha aliwahimiza vijana kufanya kazi na kutafuta makazi yao  na watoto wao badala ya kukaa wakiombea wazazi wao wafe ili waridhi mali ambazo mara nyingi huleta migogoro kwa familia kutokana na kila mmoja kugombea.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiwa msibani 


0 Comments:

Post a Comment