MWANDISHI WA habari Pascal Mayala na wahariri wa gazeti la kila wiki, la Raia Mwema wanaotakiwa kuhojiwa na kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge Kwa madai ya kuchapisha habari inayodhalilisha bunge, Aprili 9, mwaka huu.
Hayo yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai amelieleza bunge leo kuwa habari huyo ilidhamiria kuchafua hadhi ya bunge.
Spika Ndugai aliyasema hayo baada ya mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga kuomba mwongozo wa Spika juzi Aprili 9, akihoji iwapo habari iliyoandikwa na gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Bunge linajipendekeza?” haidhalilishi bunge.
Spika Ndugai leo Aprili 12, ameliambia bunge kuwa mwandishi huyo na wahariri watatakiwa kuhojiwa na kamati hiyo ya bunge.


0 Comments:
Post a Comment