SABABU ZA RAIS KUBADILI MPAMBE WAKE HIZI HAPA


RAIS John Magufuli ameridhia na kuwapandisha vyeo maofisa 28 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiwemo Mpambe wake Kanali Mkeremi ambaye sasa anakuwa Brigedia Jenerali hivyo kwenda kupangiwa kazi nyingine jeshini.

Aidha, Rais pia ameridhia kumpandisha cheo Luteni Kanali D.P.M Murunga kuwa kanali hivyo kuwa mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Mkeremi.

Akitoa taarifa ya uteuzi huo leo Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi na kwamba maofisa wote hao watavalishwa vyeo vyao Ijumaa hii katika makamo makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es salaam.

Katika uteuzi huo Rais Magufuli amewapandisha vyeo maofisa wa ngazi mbalimbali Jeshini ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini

0 Comments:

Post a Comment