MASOGANGE KUZIKWA MBOZI, ANAAGWA LEO LEADERS CLUB

Video queen maarufu Bongo Agnes Gerald "Masogange" anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao wilayani Mbozi, mkoani  Mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko.

Dada wa Agnes,Emma Gerald, amewaeleza waandishi wa habari jana kuwa mwili wa Marehemu  Agnes utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni leo Jumapili kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Ambapo misa itafanyika viwanjani hapo kisha kuanza safari rasmi kuelekea Mbalizi mkoani Mbeya kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa marehemu Agnes Gerald mahali pema peponi.
“Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald.
Aidha imeelezwa kuwa kutakuwa na mabasi mawili yatakayobeba wasindikizaji wa mwili huo mpaka mkoani Mbeya.
Agnes Masogange amefariki jana Aprili 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pumu.

0 Comments:

Post a Comment