SIRI MAUAJI NDOGO WAKE MBUNGE HECHE YABAINIKA



BAADA ya wananchi wa Tarime kuzingira kituo cha polisi kufuatia mdogo wa mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini John Heche, Suguta Heche kuuawa kwa kuchomwa kisu na polisi hatimaye jeshi hilo limekiri askari wake kuhusika.

Kamanda wa polisi kanda maalum Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha kuuawa kwa Suguta kwa kuchomwa kisu na Polisi.

Amesema  marehemu alikuwa na mgogoro na mmoja ya askari waliokuwa wamemkamata, na kufikia hatua ya kutaka kushikana (kupigana) ndipo askari aliposhindwa kujizuia na kumchoma kisu.

“Tukio ni la kweli limetokea na huyo askari tunamshikilia, huyo kijana alikamatwa usiku sasa wakati wapo kwenye gari wakielekea kituo cha polisi, ukatokea mzozo kati ya huyu askari na huyu marehemu, mzozo kama wanataka kupigana, mwenzake akaingilia kuamua," amesema kamanda Mwaibambe na kuongeza.

" Lakini ni kweli askari amemjeruhi huyu mgongoni, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi leo saa 6 mbele ya ndugu zake, kweli umekutwa na jeraha la hicho kisu mgongoni na mtuhumiwa alikuwa hajavalishwa pingu, ila hatujui nini waliambiana mpaka kufikia hivyo”,.

 Kamanda Mwaibambe amesema hali ya kituoni hapo kwa sasa imetulia baada ya wananchi kufurika kulalamikia mauaji hayo, na kwamba amezungumza na ndugu wa familia kuwaeleza jinsi tukio lilivyokuwa.


0 Comments:

Post a Comment