Mahakama ya Juu nchini Guine ya Ikweta imethibitisha kufutwa kwa chama kikuu cha upinzani, Citizen’s for Innovation (CI), huku ikiridhia kifungo cha miaka 30 jela kwa wafuasi wake ishirini na moja akiwemo mbunge pekee wa chama hicho.
Kwa mujibu wa mtandao wa Africanews awali uamuzi huo ulifanywa na mahakama ya jimbo la Mongomo mnamo Februari 26, 2018 kwa makosa ya uchochezi, uvunjifu wa amani, shambulio kwa vyombo vya dola.
Tayari Rais wa nchi hiyo ametoa pongezi kwa mahakama na kutaka wananchi kufuata utawala wa sheria na kuheshimu maamuzi ya mahakama.
Mashitaka dhidi ya chama hicho yalitokana na vurugu pamoja na maandamano yaliyofanywa na chama hicho wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu kwenye maeneo ya Aconibe, mji ambao ni nyumbani kwa kiongozi wa chama hicho Bwana Gabriel Nse Obiang Obono
SOURCE: Africanews
0 Comments:
Post a Comment