Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani imemuachia huru, kijana Frank Joseph (23) aliyeiba kiroba cha Mahindi debe 1 na kumnasia kichwani baada ya mlalamikaji, Seve Seleman kutofika mahakamani hapo mara 3 mfululizo.
Uamuzi huo umetolewa jana Mei 16, mwaka huu na Hakimu Mfawidhi, Nabwike Mbaba wakati shauri hilo lilipofika mahakamani hapo kwa ajili mlalamikaji (mtendewa) kutoa maelezo ya jinsi alivyoibiwa.
Hakimu Mbaba amesema kuwa kutokana na mlalamikaji, Seve kushindwa kufika mahakamani hapo mara 3 mfululizo kutoa maelezo ya kuibiwa kwake anaifuta kesi huyo.
“Mtendewa ameshindwa kufika mahakamani licha ya kupewa wito mara 3 mfululizo, hivyo naifutilia mbali kesi hii na mshtakiwa kuanzia sasa upo huru,” amesema Hakimu Mbaba.
Awali mshtakiwa alishindwa kufikishwa mahakamani mara 2 mfululizo kutokana na gari la Magereza kuharibika.
Katika kesi hiyo namba 124/2018 Frank mkazi wa Mbezi anadaiwa mnamo Mei 3, mwaka huu majira ya saa 7 usiku maeneo ya Mlandizi aliiba Mahindi debe 1 likiwa na thamani ya Sh.20, 000 mali ya Seve Seleman
0 Comments:
Post a Comment