Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, DK Harrison Mwakyembe
Amri hiyo imetolewa lei kufuatia maombi yaliyowasilishwa na Jamii Media, Taasisi ya msaada wa sheria na utetezi wa haki za binadamu, (LHRC), Umoja wa asasi zisizo za kiserikali za utetezi wa haki za binadamu, (THRDC), Baraza la Habari nchini, (MCT), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake,( TAMWA) na jukwaa la Wahariri, (TEF).
Katika kesi ya mapitio washitakiwa ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).
Waleta maombi wanaitaka mahakama hiyo kufanyia mapitio ya kanuni hizo kwa kile wanachodai kuwa Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake (Ultra vires).
Wanadai kanuni hizo kinakiuka kanuni za usawa (Natural justice) na zinapingana na Uhuru wa kujieleza (Freedom of Expression) Haki ya kusikilizwa(Rights to be heard) na haki ya usiri( Right to Privacy)
Kesi imeahirishwa mpaka Mei 10, mwaka huu itakaporudi mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa.
Source JF


0 Comments:
Post a Comment