MSIGWA AOMBA RADHI KWA KUMSIFU JPM



MJUMBE wa kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA), Peter Msigwa ameomba radhi kwa kauli aliyotoa mbele ya Rais, John Magufuli akielezea namna anavyoendesha nchi kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo kama barabara zinajengwa bila ubaguzi wa vyama.
Msigwa ameandika kwenye ukurasa wake wa face book leo.👇🏻
“Ufafanuzi  wangu bado haueleweki na ni heshima kuzingatia maumivu yenu kwa mkanganyiko huu. Nagundua  rafiki zangu na wanachama wetu wanaugua.Basi niseme nini?Naomba nisameheni sana. The cause we are fighting for is more important than my personality. I take full responsibility”

0 Comments:

Post a Comment