MAJALIWA AELEZA SABABU IDADI ZA VIFO VYA UKIMWI KUSHUKA




 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa jana (Jumanne, Desemba Mosi, 2020) alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika uwanja wa Mandela Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.


Waziri Mkuu amesema kuwa uimarishaji wa huduma za tiba ikiwemo matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) umechangia kupunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI kutoka vifo vya watu 85,000 mwaka 2001 hadi kufikia vifo 21,529 mwaka 2019.


Waziri Mkuu amesema mbali na kupungua kwa vifo hivyo, pia maambukizi mapya ya UKIMWI nayo yamezidi kupungua kutoka watu 130,000 mwaka 2001 hadi kufikia watu 68,484 mwaka 2019, hivyo ametoa wito kwa wadau wote katika mapambano ya ugonjwa huo waongeze jitihada.

0 Comments:

Post a Comment