WAKUU wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini wmeagizwa kuunda vikundi vya mazoezi (Jogging clubs) katika maeneo yao ili kuweza kupambana na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yanayosababishwa na mtindo mbaya wa maisha.
Naibu waziri wa utamaduni Sanaa na michezo Pulina Gekul l aliyasema hayo wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza kwenye viwanja vya Sheilh Amri Abeid Arusha .
Alisema kuwa mfumo wa maisha uliopo kwa sasa ni hatari kwa afya hasa kwa watumishi wa umma kutokana na kutekeleza majukumu yao wakiwa wamekaa ofisini muda mrefu ambapo wakifanya mazoezi kwa makundi makundi mbalimbali itasaidia kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.
“Nitoe rai kwa wananchi wote na watumishi kushiriki kushiriki katika mazoezi kabla ya kazi na baada ya kazi kwani awali magonjwa haya yalikuwa kwa asilimia 20 na sasa asilimia 33 na tunategemea yatafikia asilimia 40 kama hatua madhubuti hazitachukuliwa juu ya kubadili aina za maisha kwa kufanya mazoezi lakini pia kuzingatia lishe sahihi,”Alisema Gekul.
Alifafanua kuwa magonjwa haya sio tishio tu kwa nchi ya Tanzania bali ni kwa ulimwengu wote ambapo kwa takwimu za mwaka 2016 yanasababishwa vifo milioni 41 sawa na asilimia 71 Duniani kote.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Vivian Timothy Onanji alisema kuwa kinachohitajika ili kuleta faida za kiafaya na kupunguza athari zitokanazo na tabia ya kutokujishugulisha.
Alisema kwa mara ya kwanza yametolewa mapendekezo yanayohusisha tabiabwete miongoni mwa makundi maalum kama vile wajawazito, waliojifungua,wanaoishi na maradhi sugu na wenye ulemavu ambopo lengo la mpango huo wa kidunia ni kupunguza tabia ya kutokujishugulisha kwa asilimia 15 ifikapo mwaka 2030.
Dkt Onanji alisema kuwa muongozo huo umetoa mapendekezo muhimu ya kiafya kwa watu wa rika tofauti kwanzia miaka 5 hadi 64 na zaidi bila kujali tofauti za kijinsia, tamaduni, hali ya kiuchumi na kuendelea.
Aliayataja magonjwa yasiyoambukiza yanajumuisha magonjwa ambayo hayawezi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama vile shinikizo la juu la damu, Saratani, Kisukari, Pumu, magonjwa ya akili, Siko seli, Ajali na baadhi ya magonjwa ya macho, kinywa, masikio, pia na koo.
Dkt Onanji alisema kuwa muongozo wa mazoezi umeandaliwa kufuatia uchambuzi yakinifu wa sera, sheria, kanuni na miongozo ya ushughulishaji mwili hapa nchini ambapo ulihusisha taasisi na sekta zote kutoka pande zote za Jamuhuri ya muunganao wa Tanzania.
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela Alisema kuwa kama mkoa wataendelea kuinzi na kuheshimu fursa hiyo waliyopewa na kwa wiki nzima ya maadhimisho hayo watashiriki kikmilifu ili kuweza kufikia lengo la kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.
0 Comments:
Post a Comment