DCI AMUUMBUA RC ARUSHA


 

Katika hatua nyingine DCI, Mngulu alikanusha taarifa zilizowahi kutolewa na mkuu wa Mkoa, Mulongo mwezi agosti mwaka jana kuwa polisi wamefanikiwa kukamata  wahusika wa mtandao wa walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kwenyemkutano wa wa hadhara wa Chadema, Soweto mkoani Arusha.

 

DCI aliendelea kusisitiza kuwa wao kama watendaji wa jeshi la polisi mpaka sasa hawamshikilii yeyote kuhusiana na tukio la Soweto zaidi ya mtu mmoja aliyefikishwa mahakama kuhusiana na tukio la bomu la kanisani.

 

" Msichanganye masuala ya utendaji na siasa, sisi Jeshi la polisi hatujakama mtu hayo nayodai mmelezwa na mkuu wa mkoa nendeni mkahojiane naye awaeleze hao anaodai kuwa wanahojiwa mbona hawajafikishwa mahakamani, nimesema muulizeni yeye (RC) ,huyo ni msemaji wa serikali, hayo aliyowaambia mrudieni mkamuulize yeye, sisi kama polisi hatuna taarifa kama hiyo''alisema Mngulu.

Vyombo mbalimbali vya habari vilimnukuu Mulongo wakati wa mkutano wa siku moja wa kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha, uliofanyika eneo la Olasiti akidai kuwa Polisi wako katika hatua za mwisho za mahojiano na watuhumiwa hao, ambapo mbali na kutaka kufahamu waliowatuma na malengo yao, pia wanatarajia kupata taarifa za waliorusha mabomu hayo.

 "Watuhumiwa hawa siku si nyingi Kamanda wa Polisi wa Arusha, ataweka majina hadharani, watu wawajue na si wageni, ila kwa sasa kinachochunguzwa ni kutaka kufahamu waliowatuma kuingiza mabomu hayo na kwa lengo gani," alinukuliwa mkuu huyo wa mkoa.

 

Hata hivyo Mulongo alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizo na kuulizwa juu ya jambo hilo alisikiliza kisha akakata simu bila kutoa majibu ambapo alipopigiwa tena simu hiyo ilikuwa imezimwa kabisa.

0 Comments:

Post a Comment