JUMLA ya meno ya tembo 495 yamekamtwa kwenye maeneo
mbalimbali nchini katika kipindi cha cha miezi mitatu kuanzia Januari mpaka
Machi mwaka huu.
Aidha watuhumiwa wa ujangili 544 wamefunguliwa mashtaka
kwenye mahakama mbalimbali ambapo kesi 62 zimemalizika huku 38 zikiwa bado
zinaendelea.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Paul Sarakikya
alipokuwa akitoa taarifa ya robo mwaka juu ya hali ya ujangili hapa nchini.
Alisema kuwa nyara hizo za Serikali zilikamtwa kufuatia doria iliyoendeshwa na
watumishi wao waliopo kwenye mapori ya akiba na kikosi cha kuzuia ujangili
kwenye maeneo mbalimbali.
Sarakikra alisema kuwa katika kipindi hicho jumla ya mizoga ya tembo 39 ilionekana ndani
na nje ya hifadhi za Taifa na Mapori ya akiba huku nyama za wanyamapori kiasi
cha kilo 1,111 zikikamtwa.
“Aidha meno ya tembo yaliyoakamtwa yalikuwa katika hali
mbalimbali ambapo mazima yalikuwa 171, vipande 22 vya meno ya tembo ghafi,
vipande 302 vya meno ya tembo yaliyochakatwa yenye jumla ya kilo 662.62
yalikamatwa,” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa Idara ya Wanyamapori.
Alisema kuwa pia walifanikiwa kukamata silaha 11 ikiwemo
bunduki ya rasharasha 1, Rifle 3, Shotgun 2, gobore 5 pamoja na risasi 7 za
aina mbalimbali.
“Mali na vifaa vingine vilivyokamatwa ni pamoja na magari
matano ambavyo vilikamtwa kwa kuhusika kwenye vitendo vya ujangili hasa wa meno
ya tembo, ng’ombe 2,663 walioingia kwenye hifadhi pamoja na msumeno mmoja wa
kukata mbao na mbao 745,” alisema Sarakikya.
Alisema kuwa kati ya kesi 124 zilizofunguliwa kwenye
mahakama tofauti nchini 62 zilizokuwa na
washtakiwa 85 zilimalizika kwa watuhumiwa kulipa faini ya zaidi y ash milioni
25.5.
Sarakikya alisema kuwa meno ya tembo waliyokamata
yalitokana na matukio ya siku za nyuma jambo alilodai kuwa walilibaini kutokana
na meno hayo kuwa yamebadilika rangi kwa kuchimbiwa ardhini muda mrefu huku
mengine yakimeguka.
0 Comments:
Post a Comment