SPIKA
wa Bunge la Afrika Mashariki,(EALA), Dk Magreth Banbtonbg Zziwa jana
ameahirisha bunge hilo kwa muda usiojulikana baada ya kutokea mabishano
ya kisheria baina ya mbunge na mwanasheria wa EAC, Wilberd Kahwa juu ya
hoja ya kumng’oa kwenye kiti iliyokuwa ikiwasilishwa na mbunge, Peter
Muthuki kutoka Kenya.
Aliahirisha bunge hilo wakati kikao cha jana kikiwa kimedumu kwa dakika 18 kuanzia saa
9:40 baadala ya muda wa kawaida wa saa 8:30 na kuahirishwa saa 10:03
ambapo mkutano huu ulitajariwa kumalizika april 4, mwaka huu.
Mabishano hayo ya kisheria yalikuwa baina ya Mwanasheria huyo wa EAC na Mbunge
kutoka Uganda Dk. Fred Mbide aliyetaka muongozo wa spika akitaka hoja
ya kumng’oa spika isijadiliwe mpaka kesi aliyofungua kwenye mahakama ya
Afrika Mashariki,(EACJ) imalizike.
Kahwa
kwa nafasi yake ya uanasheria wa EAC alijaribu kutolea ufafanuzi suala
hilo huku akitumia vipengele mbalimbali vya mkataba uliounda jumuiya
pamoja na kanuni zinazosimamia bunge hilo kuonyesha kuwa hoja hiyo
inaweza kuendelea licha ya kuwepo kwa shauri mahakamani kwani sheria
iliyopo inawabana wakuu wan chi wanachama.
Hata
hivyo spika Zziwa kwa kutumia mamlaka yake kikanuni alisema kuwa
anaweza kuchagua njia ya kupatia ufumbuzi suala lolote linalokuja mbele
yake huku akidai kuwa kwa kuwa wao ni watunga sheria ni vema wakaachana
na suala hilo hivyo akaamua kuahirisha bunge hilo kwa muda usiojulikana
majira saa 10.03.
Hata
hivyo baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho wakati Spika akitoka kwenye
ukumbi wa bunge wabunge wengi hawakusimama kama kanuni zinavyowataka.
Spika
Zziwa baada ya kutoka kwenye ukumbi huo wa bunge aliingia kwenye ofisi
yake iliyo karibu na ukumbi huo na kubadili mavazi ya spika, joho na
kofia kisha akaelekea moja kwa moja kwenye gari lake na kuondoka kabisa
kwenye eneo hilo.
Hali
hiyo iliwafanya badhi ya wabunge walio wengi wanaotaka spika ang’oke
kurudi kwenye ukumbi wa bunge na kujifungia kwa kile kiliochoelezwa kuwa
ni kutafuta njia ya kushughulikia suala hilo.
Tokea kuanza kwa mkutano huu wa bunge Mach 25, mwaka huu kumekuwa na harakati mbalimbalivikao
Hoja ya kung’olewa kwa spika huyo inaungwa mkono na wabunge wote kutoka
Rwanda na Burundi wamesaini kuridhia hoja hiyo huku watano kutoka Kenya
na Tanzania nao wakisaini kukubaliana na hoja hiyo ambapo Uganda
anakotokea spika huyo wabunge watano walisaini kuridhia kung’olewa kwa
spika huyo.
Hata hivyo kabla ya kuanza kikao cha jana wabunge walikuwa na mgomo
baridi wa kuingia kwenye ukumbi wa bunge hali iliyolazimu ofisi ya
spika kubadili ratiba ya shughuli za bunge ambapo wasaidizi wa Katibu wa
bunge, Keneth Madete walionekana kubadili karatasi zilizokuwa zimewekwa
na kuwekwa zile zinazohusiana na hoja ya kumtoa spika kwenye kiti.
Kwa
mujibu wa kanuni ya tisa ya inayosimamia bunge hilo inaeleza kuwa baada
ya hoja ya kumuondoa spika kuwasilishwa kwa katibu wa bunge inatakiwa
ijadiliwe bungeni ndani ya siku saba ambapo wakati kamati ikuchunguza
madai yanayompelekea kuondolewa spika anaweza kusimama mwenyewe , kuweka
mwanasheri au mtu yeyote kumwakilisha.
Kanuni
hiyo inaeleza kuwa spika atapisha kwenye kiti kuruhusu uchunguzi huo
ambapo ili kumng’oa itapigwa kura ambapo inatakiwa iungwe mkono na
theluthi mbili ya wabunge wote 45 walio kwenye bunge hilo.
Madai ya msingi ya wabunge hao yaliyowasukuma kumkataa Spika
Zziwa ni kuwa amepwaya kwenye nafasi hiyo kwani ameshindwa kutimiza
majukumu yake ipasavyo hali kutokana na udhaifu mkubwa wa kiuongozi
alionao ambao hauzingatii utawala bora.
Madai
mengine ni matumizi mabaya ya ofisi, kutowaheshimu na kuwabagua
wafanyakazi na wabunge mambo yaliyopelekea wabunge kukosa imani naye.
Mwanzo mwa wiki iliyopita Mwenyekiti wa
Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uhuru Kenyatta alilamizimika
kufanya kikao cha dharura na wenyeviti wa wabunge toka nchi tano
zinazounda jumuiya hiyo kwa kile kilichodaiwa ni kujaribu kutuliza
harakati za wabunge hao kutaka kumng’oa Spika, Dk. Banbtonbg Zziwa.
Kikao
hicho ambacho hakikuwa kwenye ratiba iliyotolewa asubuhi ya siku hiyo
kilifanyika mara baada ya Rais Kenyatta kumaliza kuongea na waandishi
ambapo muda huo alitakiwa kushiriki chakula cha mchana na wabunge wa
EALA.
Kikao
hicho kilichofanyikia kwenye ofisi ya spika kilidumu kwa dakika 40
ambapo alipomaliza alitoka na kuwapungia mkono wabunge na wafanyakazi wa
jumuiya hiyo na kuondoka huku wabunge wa EALA waliokuwa eneo hilo
wakionekana kuweka mkakati wa pamoja kuhakikisha hawabadilishi msimamo
wa kumng’oa spika.
0 Comments:
Post a Comment