NYALANDU APUUZA TUHUMA ZA KUUZA KATAVI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amepuuzia tuhuma zilizoelekezwa kwake kuwa ameuza Hifadhi ya Taifa ya Katavi imeuzwa na inatarajiwa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini.

Amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli hata chembe kwani wizara yake haiwezi na wala haina mpango wa kuuza hifadhi yoyote wala maeneo yote yaliyo chini yake.

Waziri huyo wa Maliasili na Utalii alisema kuwa huenda huo ni mkakati wa majangili kutaka kubadili mwelekeo wa vita ya kukabiliana nao kwa kutumia baadhi ya waandishi wa habari kutoa habari za kupotosha umma hali itakayoifanya Serikali kujikita kujibu tuhuma hizo za uongo hivyo kuwapa wao fursa ya kuendelea na ujangili.

“Nadhani uandishi huu wa habari hauna thamani ya wino katika kalamu, kuweza kuandika uongo kama huo, Serikali ya Tanzania sio kwamba tu haiuzi hifadhi ya aina yoyote lakini  hatuuzi pori.
“Hawa watu naweza kusema ni sehemu ya majangili ambao kutokana na vita tunayowapiga  wanaamua kutafuta waandishi wa habari uchwara na kuwatumia kuandika habari za uongo, aliyekuambia  Serengeti imeuzwa ni nani au anasema Katavi imeuzwa ni nani, imeuzwa bei gani, mnunuzi ni nani  na manunuzi hayo yamefanyika wapi na Watanzania walikuwa wapi?” alihoji Waziri Nyalandu.

0 Comments:

Post a Comment