WATU
sita wanaodhaniwa kuwa ni majangili wamekamatwa na meno ya tembo 53
yenye jumla ya kilo 169.7 wakiwa na silaha aina ya SMG yenye magazine
tatu kwenye kijiji cha Kiomboi wilayani Manyoni Mkoani Singida .
Aidha Jumla ya tembo 26 wameuawa na majangili kwenye mapori ya akiba ya Rungwa na Kizigo yaliyopo wilayani humo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyasema hayo April Mosi, mwaka huu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
Alisema
kuwa majangili hao walikamatwa juzi majira ya saa 6:00 usiku na kikosi
kazi maalum cha kukabiliana na ujangili kanda ya kati – Manyoni ambapo
wanashikiliwa kwenye kituo cha polisi Manyoni.
“Msako
zaidi unaendelea ili kuwakamata watu wote waliohusika na mtandao wa
mauaji ya tembo hao 26 na Serikali inawaomba wananchi wenye taarifa
kuhusu uhalifu huo wasisite kutoa ushirikiano kwa askari wa wanyamapori,
jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.” alisema Nyalandu.
Hata
hivyo hakuwa tayari kuyataja majina ya watuhumiwa hao wa ujangili kwa
madai kuwa hatua hiyo inaweza kukwamisha jitihada za kuwakamata
washirika wao.
“Hawa
tunaowashikilia inawezekana ni wabebaji tu, hawa watu huwa wanamitandao
mipana sasa tunaendelea kusaka wenzao wakiwemo wale wanaowatuma na
wasafirisha hivyo naomba nisitaje majina yao kwa sasa kuepusha hao
wengine kutoroka,” alisema Nyalandu.
0 Comments:
Post a Comment