Saini za Nyerere na Msekwa kwenye
hati hizo, Nahodha alisema yeye siyo mtaalamu wa maandishi kubaini kuwa
hati hizo na saini zake ni halali au la.
Hata hivyo, alisema Msekwa alikiri kwenye kamati hiyo kuwa saini iliyopo kwenye hati ya makubaliano ya Muungano ni yake.
Utata wa saini za Msekwa uliibuliwa na baadhi ya
wajumbe ambao walihoji tofauti baina saini iliyopo kwenye sheria hati ya
muungano na saini zake katika nyaraka nyingine rasmi.
Wajumbe waliombana Msekwa wakiongozwa na Godbless
Lema, pia walitilia shaka matumizi ya kompyuta katika sheria hizo
zilizoandikwa mwaka 1964.
“Mwaka 1964 hakukuwa na kompyuta lakini hapa
tunaona sheria zimeandikwa kwa kompyuta na hata sehemu ya saini ya
Msekwa na Nyerere kuna herufi zimeandikwa kwa kompyuta,” alinukuliwa
Lema.
Katika maelezo yake Msekwa licha ya kukiri
upungufu, aliwakumbusha wajumbe kuwa siku ya kusainiwa hati hizo, picha
zilipigwa na zipo hadi sas
0 Comments:
Post a Comment