Namnukuu Rais Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa CCM Taifa 'Ni utovu wa nidhamu
na ukosefu wa adabu kumtukana na kuwakejeli waasisi" Kisha naendelea
kunukuu "Misingi aliyoacha ndiyo inayoendelea kuongoza nchi na siku
tukiiacha nchi itaingia kwenye matatizo.Marais wote kuanzia Mzee
Mwinyi,Mkapa na hata Mimi tumeendelea kuifuata misingi hiyo".
Naomba kuhoji .Ni nani anayemtukana na kumkejeli Baba wa Taifa hapa
Unafiki pembeni sasa.Je misingi ya kuzika azimio la Arusha ndiyo
inayojenga heshima kwa Nyerere?
Je Nyerere anaheshimika kwa Rais Mkapa Kuruhusu uuzaji wa Benki ya NBC
tena benki ya Umma kwa Shilingi Milioni chache tu(Bei ya Kutupwa) kwa
mabepari wa Kikaburu?
Je,Nyerere anaheshimika na kuenziwa kwa Mkapa kujimilikisha Mradi wa
Kiwira (Tuhuma ambazo sijawahi kusikia au kuona akikana)?
Je,Nyerere anaenziwa kwa Rais Mkapa kuongoza nchi ambayo Zaidi ya
Bilioni 100 na ushehe kuchotwa Benki Kuu bila yeye kujua?
Je,ni heshima kwa Nyerere na misingi yake kuruhusu wezi wa EPA
kurudisha fedha walizoibia umma bila hatua za kisheria ?Kwamba Nyerere
aliwahi kujivunia kufanya majadiliano na wezi na mafisadi wa mali za
umma?
Je,Nyerere hatukanwi kwa tawala za Rais Mkapa na Kikwete kuruhusu
Dhahabu kuchimbwa kwa misamaha holela bila kulipa kodi huku wananchi
hasa Geita wakigeuzwa kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao bila vita?
Je,Misingi ya Nyerere ndio iliyoruhusu vijana kugeuzwa manamba kwenye
makampuni ya madini huku wakifa vifo vya kikatili kutokana na
mazingira hatarishi ya kufanya kazi?
Hivi tamko hili sio kejeli kwa baba wa Taifa na misingi yake?
Ujamaa na kujitegemea ndio msingi wa Taifa letu.Je Taifa letu na hata
chama tawala alichokiasiasi Mwl.Nyerere kinafuata misingi hiyo?
Je,CCM ni chama kinachotetea maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi
wanaokatwa kodi Asilimia 18 na Zaidi ya mishahara kiduchu huku
mabepari waliowekeza kwenye Migodi yetu wakipata misamaha ya kodi na
wengine kuwezeshwa kukwepa kodi?
Ni nani anayemkejeli Mwalimu Nyerere hapa?
Washauri wa Rais Ikulu walitakiwa kumshauri Rais kabla ya kutoa Tamko
ambalo litaamsha hasira na hisia za uchungu miongoni mwa jamii ya
Watanzania
Ikulu na Rais Kikwete aombe radhi kwa taarifa hii ya uongo na
upotoshaji ili kulinda heshima yake yeye,chama chake na Ikulu.
Imeandikwa na Ben Saanane
0 Comments:
Post a Comment