WAPAMBE wa wagombea kwenye uchaguzi wa Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM), Wilaya ya Arusha wamechapana makonde hadharani baada ya kutofautiana lugha wakati wakiingia ukumbini.
Purukushani hiyo ilitokea jana majira ya asubuhi na kudumu kwa zaidi ya dakika 20 wakati wajumbe wakiingia kwenye mkutano huo uliofanyikia kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Rose kabla mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro hajawasili.
Hali hiyo iliwalazimu kampuni Ultimate security
wanaolinda hoteli hiyo kuimarisha ulinzi kwa kuongeza gari lenye idadi kubwa ya walinzi na vifaa ili kuhakikisha wapangaji na watumiaji wengine wa jengo hilo wanakuwa salama.
Inadaiwa kuwa kilichopelekea kuibuka kwa vurugu hizo ni baada ya wapambe kutuhumiana kuwa kuna matapeli kwenye kambi za wagombea wa nafasi ya uenyekiti zilizokuwa zinawaniwa na Jimmy Pamba na Godliving Kisila.
Inadaiwa kijana wa kambi ya Kisila,Hussein Abdallah alimtuhumu mwenzake,Lameck Dudu ambaye yuko kambi ya Pamba kuwa eneo la uchaguzi wakati si mjumbe halali wa mkutano huo na huku akimwita kuwa tapeli la kisiasa.
Kauli hiyo haikumfurahisha Dudu ambapo aliamua kurusha konde zito lililompata kisawasawa Husein na kupelekea kudondoka chini.
Hali hiyo ikawaibua wapambe wa pande zote ambao walianza kurushiana Makonde ambapo kwenye eneo hilo alikuwepo askari mmoja wa kike wa kikosi cha kituliza ghasia (FFU), ambaye alijaribu kuwamua bila mafanikio.
Inaelekea alitoa taarifa polisi kwani gari la polisi liliwasili likiwa na Idadi kubwa ya askari ndipo wakafanikiwa kurejesha hali ya amani kwenye eneo hilo.
Mmoja wa vijana aliyekutwa na zahama hiyo na kuchaniwa nguo zake pamoja na
kupata kibao, Silvester Meda alisema
hajui kosa alilotenda mpaka astahili kupatiwa kipigo hitching.
Meda alidai UVCCM Arusha imezungukwa na wahuni, hivyo chama kinapaswa
kuwachukulia hatua wote walioiabisha Jumuiya hiyo kwa maslahi yao.
Katibu Hamasa wa UVCCM Wilaya ya Arusha,Abdi Marijana aliwataka polisi kumkamata Dudu kwani ndiye
aliyesababisha vurugu hizo kwa kufika kwenye mkutano huo wakati akijijua si mjumbe.
‘’Dudu alipaswa kukamatwa kwani ndiye aliyeleta vurugu kwa kumpiga
ngumi Hussein Abdalla, lakini polisi hawakufanya hivyo hilo mie sijui
ni kwa nini,’’alisisitiza.
0 Comments:
Post a Comment