SHOZA NA MPENZI MWINGINE MWANAMKE WALIVYOTIWA NGUVUNI NA POLISI KWA TUHUMA ZA MAPENZI YA JINSIA MOJA

 MWANAMKE anayedaiwa kuvishwa pete ya uchumba na  mwanamke mwenzake Janeth Shonza (25),amekamatwa na jeshi la polisi akiwa amejificha maeneo ya Puma mkoani Singida.


Shoza  ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza anadaiwa kuvishwa pete na  Milembe Suleiman (36), ambapo picha za tukio hilo zilisambaa mitandaoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema wanawashikilia watu wengine wawili kuhusika na tukio hilo akiwemo Richard Fabian (28), mkazi wa Buzuruga jijini Mwanza aliyepiga na kusambaza mitandaoni picha za wanawake hao wakivishana pete mitandaoni.

Mwingine anayeshikiliwa kuwa ni Aneth Mkuki (24), mkazi wa Nyasaka jijini Mwanza, mpenzi mwingine wa Janeth aliyemsaidia kutoroka kukwepa kutiwa mbaroni na polisi baada ya video yao kusambazwa mitandaoni.

Kamanda Msangi alisema watuhumiwa hao watafutie mahakamani mara upelelezi yatakayosomwa.

0 Comments:

Post a Comment